Babutale ni meneja maarufu wa kundi la bongofleva la Tip Top connection lakini pia ni meneja wa mwimbaji Diamond Platnumz ambapo leo Tale ameguswa na baadhi ya video kadhaa za bongofleva baada ya kuzitazama akaandika haya.
Hii ni kwa ndugu zetu madirector wa nyumbani tanzania, tunaomba angalau muwe mnajishugulisha kuangalia vitu ambavyo havijatumika ili kuepuka kufananisha video zetu,sababu inapelekea wasanii kukimbia na kwenda kufanya kazi zao nje ya nchi
Mfano kuna video ya dogo janja na roma zote location moja,madee bilnas na wengine wote wametumia vitoa moshi,chege na ben paul wote wametumia gari moja,hilikosa ni la msanii au director? #kelele_za_chura@chegechigunda
No comments: