» » Picha/Video: Gorilla aliyeuawa baada ya mtoto kuangukia kwenye zoo azua mjadala duniani

Walinzi wa zoo waliompiga risasi na kumuua gorilla Jumamosi baada ya mtoto wa kiume mwenye miaka minne kuteleza na kuangukia kwenye eneo lenye mawe na maporoko ya maji alilokuwa akitunzwa huko Cincinnati, Marekani wamesababisha mjadala na hasira kali duniani kutokana na uamuzi huo.

34BD01DF00000578-3615783-The_zoo_shot_the_beloved_animal_after_he_dragged_the_boy_through-a-3_1464591377084

Familia hiyo ilienda kutembea kwenye zoo hiyo Jumamosi iliyopita na ndipo mtoto wao alipoteleza na kuanguka kwenye eneo alipokuwa mnyama huyo. Mtoto huyo alichukuliwa na kupelekwa kwenye hospitali ya watoto na kuruhusiwa jioni ya siku hiyo.
Familia hiyo ilitoa shukrani kwa waangalizi wa zoo hiyo.
“We are so thankful to the Lord that our child is safe. He is home and doing just fine. We extend our heartfelt thanks for the quick action by the Cincinnati Zoo staff. We know that this was a very difficult decision for them, and that they are grieving the loss of their gorilla. We hope that you will respect our privacy at this time.”
Baadhi ya watu wanadai kuwa wazazi wa mtoto huyo wanapaswa kukamatwa kwa uzembe wao.

34C650F800000578-3616453-image-a-56_1464634975377

Ombi la mtandaoni (petition) lililopewa jina ‘Justice for Harambe’ limepata sahihi zaidi 100,000 ndani ya saa 48. “This beautiful gorilla lost his life because the boy’s parents did not keep a closer watch on the child,” inasema petition hiyo.

34C655C300000578-3616453-image-a-54_1464633222408

Na sasa mtandao wa Daily Mail umebaini wazazi wa mtoto huyo kuwa mama yake Michelle Gregg, 32 na mume wake Deonne Dickerson, 36, mwanaume ambaye inasemekana ana historia ya matukio ya kihalifu.

34C8870D00000578-0-image-a-1_1464652047487

Makosa aliyowahi kutuhumiwa kufanya ni pamoja ujambazi, makosa ya kutumia silaha za moto, biashara ya madawa ya kulevya na mengine.

About toooo yoooo

Hi there! I am Hung Duy and I am a true enthusiast in the areas of SEO and web design. In my personal life I spend time on photography, mountain climbing, snorkeling and dirt bike riding.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply