Friday, 3 June 2016

Video: Keki yakatwa kumkaribisha Rich Mavoko ‘State House’ ya Diamond

Baada ya Rich Mavoko Alhamisi hii kuandika historia mpya katika maisha ya muziki wake kwa kusaini rasmi mkataba wa miaka 10 wa kufanya kazi na label ya ‘WCB’ iliyochini ya Diamond Platnumz, staa huyo wa hit nyingi amekaribishwa rasmi ‘State House’ ya Diamond iliyopo Madale kando kando kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Rich Mavoko akaribishwa kwa shangwe State House

Kwa mujibu wa mmoja kati ya viongozi wake WCB, alikiambia chanzo kuwa tukio hilo haliitaji maparazi kwani wameliweka kifamilia zaidi. Hata hivyo Diamond ali share hata video kwa mashabiki wa muziki wake kuonyesha namna walivyompokea msanii huyo.
Kwa sasa Rich Mavoko anatamba na video yake mpya ya wimbo ‘ibaki stori’ ambayo ilizinduliwa jana baada ya kusaini mkataba na WCB.

No comments:

Leave a Reply